Dar es Salaam, Tanzania. Serikali awali ilitangaza mishahara mipya kwa watumishi wa umma na kufichwa, lakini sasa mishahara hiyo ya kila sekta mbalimbali imechapishwa kwenye gazeti moja la leo.
Kima cha chini kimeongezwa kwa asilimia 41.18 kutoka Sh170,000 mpaka Sh240,000 wakati mishahara ya watumishi wengine imeongezwa kwa wastani wa asilimia 8.41.
Waraka namba moja kwa watumishi wa umma kwa ajili ya mishahara hiyo ulitolewa na Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi Julai 2, mwaka huu na kueleza kwamba marekebisho hayo yanahusu watumishi wa serikali kuu na watumishi wa serikali za mitaa.
Walimu
Katika sekta ya elimu, mshahara wa kima cha chini kwa walimu kimepanda kutoka Sh223,000 mpaka Sh296,000.
Wakaguzi
Mshahara kwa wakaguzi katika ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (SAIS) kima cha chini kimepanda kutoka Sh187,000 mpaka Sh249,000.
Sekta ya Kilimo
Mshahara katika sekta ya kilimo na mifugo kwa watafiti kima cha chini cha mshahara kimepanda kutoka Sh890,300 hadi Sh916,000.
Bunge
Kwa upande huo kima cha chini cha mshahara kimepanda kutoka Sh170,000 hadi Sh240,000.
Serikali Kuu
Upande wa wafanyakazi wa serikali kuu, mshahara wa kima cha chini umepanda kutoka 170,000 mpaka 240,000.
Mwanasheria Mkuu
Katika upande wa mwanasheria mkuu, kima cha chini cha mshahara kimepanda kutoka Sh310,000 hadi Sh360,000.
Mahakama
Hapa mshahara wa kima cha chini umepanda kutoka Sh469,000 hadi Sh510,000
Sekta ya Afya
Kwa wafanyakazi wa sekta ya afya nchini, mishahara kima cha chini imepanda kutoka Sh221,500 hadi Sh261,000.
Hiyo ni mshahara ya wafanyakazi wa umma kwa taarifa zaidi soma gazeti la mwananchi.
Chanzo: Mwananchi.