BASI LA NAJMUNISA LAPATA AJALI NA KUUA WANNE PAPO HAPO


Picha na Maktaba 
 
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba basi la Najmunisa linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza limepata ajali eneo la Mbande mkoani Dodoma na kuua watu wanne na kujeruhi abiria kadhaa.
 
Basi hilo lililokuwa linaelekea Mwanza lilipata ajali hiyo baada ya kupasuka tairi la mbele. 
 
Mashuhuda wa tukio hilo wanadai kuwa mali zote za abiria ziko salama kutokana na uwepo wa Check Point ya polisi jirani na eneo la ajali. 
 
Chanzo: Radio One


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo