Sukuma wiki.
Na SAMUEL KARANJA
MWANAMUME mmoja amefikishwa katika mahakama moja ya Murang’a Kenya na kushtakiwa kwa kuiba sukumawiki za thamani ya Sh100.
Mshtakiwa Peter Gichuhi Gitau
alikanusha kuwa aliiba mali hiyo ya Bi Elizabeth Mwangi katika kijiji
cha Kiria kaunti ya Murang’a.
Hakimu mkuu mwandamizi Bw Joseph Masiga alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh50,000 au pesa taslimu Sh10,000.
Katika mahakama iyo hiyo,mwanamume mwingine alishtakiwa kwa kumnajisi msichana wa umri wa miaka 14.
Vile Vile Bw Ernest Maina Mbogo
alishtakiwa kwa kumpapasa sehemu za siri msichana huyo wa shule. Hata
hivyo alikanusha mashtaka hayo mawili.
Kiongozi wa mashtaka Bw Solomon
Nalikha aliomba mahakama kutomwachilia mashtakiwa kwa dhamana yeyote na
iwapo mahakama ingefanya hivyo, basi impe wadhamini wawili.
Hakimu alimwamchilia Bw Mbogo kwa
dhamana ya Sh500, 000 na wadhamini wawili wa kiasi kama hicho. Kesi hiyo
itasikizwo Agosti 20 mwaka huu.
Bastola
Katika mahakama hiyo, wanamme wengine wawili walistakiwa kwa makosa ya kumiliki bastola kinyume cha sheria.
Bw John Muru Ndegwa kwa jina jingine
Paul Irungu Macharia na Cyrus Kibunja Ndung’u au John Mwangi Irungu
walikanusha mashtaka hayo na kuwachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 kila
mmoja na mdhamini wa kiasi kama hicho.
Bw Ndegwa vile vile alishtakiwa kwa
kosa la kukosa kitambulisho cha taifa na kupigwa faini ya Sh15,000 au
kufungwa jela miezi18 akishindwa kulipa.