Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha
Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni s/o Sandu, miaka 20,
Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani
na Tolo s/o Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu
Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi Diwani Athumani
anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha
sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa
njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Signed by, [Diwani Athumani – ACP] kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi