ALIYEIBA SH. 30,000 ZA MKEWE AFUNGWA JELA MIAKA MITATU

Mji wa Nyahururu
Barabara ya Koinange mjini Nyahururu

Na KNA

MWANAMUME aliyeiba Sh30,000 kutoka kwa mkewe alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu na mahakama moja mjini Nyahururu.
Patrick Nderitu alifikishwa mbele ya hakimu mkuu, Bw Dennis Mikoyan na kukubali kuwa alimwibia mkewe, Bi Damaris Wanjiku katika kijiji cha Gatundia, Laikipia Magharibi nchini Kenya mnamo Mei 30, mwaka huu.

Upande wa mashtaka uliiarifu mahakama kuwa asubuhi hiyo, mkewe mshukiwa aliacha mkoba wake nyumbani kwao baada ya kuondoka kwenda kazini. Mwanamke huyo huwa ni mhudumu wa benki ya Equity katika kituo cha kibiashara cha Gatundia.

Aliporudi kuuchukua mkoba wake, hakumkuta mumewe, ambaye alikuwa ametoroka na mkoba huo ambao ulikuwa na pesa hizo. Aliacha ujumbe mfupi uliosema kuwa 'alikuwa ameenda kutafuta mahali pazuri pa kukaa'.

Ujumbe huo ulieleza kuwa mshukiwa angerudi baadaye na kumweleza mwanamke huyo kuwalea watoto.

Mwanamume huyo alirudi mnamo Julai 13, bila pesa hizo ambapo alikamatwa na kushtakiwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo