Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Ommy Dimpoz amewashukia wamiliki wa mitandao ya kijamii hasa bloggers kwa kuandika habari ambazo hawana uhakika nazo
Ommy ameyasema hayo wakati akihojiwa leo katika kipindi cha hot mix kinachorushwa na kituo cha EATV wakati akizungumzia uvumi wa mambo mbalimbali yanayomhusu yeye
"Mfano mzuri ni kwenye kifo cha Ngwea, taarifa ya hospitali haijatolewa lakini bloggers wameshaandika ripoti zao za uongo mitandaoni, sasa maana yake ni nini, Ommy dimpoz yupo kama una chochote kuhusu yeye mpigie simu umuulize atakueleza ukweli na uataandika kitu chenye uhakika" alisema Dimpoz
Pia Dimpoz amesema suala la yeye na Vanesa Mdee kupewa tuzo yake kupitia wimbo walioshirikiana wa Me & U katika kinyang'anyiro cha tuzo za Kili 2013 haoni kama lina shida kwa kuwa kila mmoja aliimba na ushirikiano wao ndiyo uliosababisha kupatikana kwa tuzo hiyo hivyo kila mmoja atapewa ya kwake
