skip to main |
skip to sidebar
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASIMU YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KARIMJEE DAR LEO

Makamu
wa Rais Dokta Mohamed Gharib Bilal amezindua rasimu ya Katiba mpya
inayopendekeza kutovunjika kwa muungano na kuwepo na serikali tatu
ambazo ni Serikali ya Shirikisho, Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Mengine
yaliyopendekezwa kwenye rasimu hiyo ni Spika wa Bunge na Naibu Spika
wasitokane na wabunge na kwamba wasiwe viongozi wa Vyama vya Siasa.
Ni katika uzinduzi wa Rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Mchakato wa Katiba Mpya Jaji
Mstaafu Joseph Warioba anabainisha mapendekezo ya Tume hiyo yaliyotokana
na maoni ya wananchi kuhusiana na suala la muungano.
Mapendekezo mengine katika rasimu hiyo ni kutokuwepo na Viti maalumu na
ukomo wa ubunge kwa awamu tatu huku wananchi wakipewa fursa ya kumuondoa
madarakani mbunge aliyechaguliwa iwapo hawataridhika na utendaji wake.
Suala la mgombea binafsi limependekezwa katika rasimu hiyo kuanzia
ngazi ya Kitongoji hadi Urais na Baraza la mawaziri lisitokane na
wabunge waliochaguliwa na wananchi.
Akizindua Rasimu hiyo
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal amewataka watanzania kutokuwa na
jazba na badala yake kupitia rasimu hiyo kikamilifu na kutoa
mapendekezo yatakayosaidia upatikanaji wa katiba yenye kukidhi mahitaji
ya watanzania.
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Angela Kairuki ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wanazungumziaje rasimu hiyo?
Rasimu hiyo imependekeza Tume ya Uchaguzi ibadilishwe na kuwa Tume huru
ya Uchaguzi na kwamba majukumu yake yaunganishwe na Msajili wa Vyama
vya siasa na mgombea wa urais atakayeshindwa ana haki ya kuhoji matokeo
kwa Tume iliyomtangaza Rais ndani ya mwezi mmoja na kupatiwa ufumbuzi.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi