HARUNA MOSHI 'BOBAN' AJIUNGA RASMI NA COASTAL UNION


 
Boban akisaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Coastal Union.
Boban (kushoto) akiwa ndani ya jezi ya Coastal Union akisalimiana na kocha wa timu hiyo, Hemed Moroko.

Hatimaye aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Haruna Moshi 'Boban' amesajiliwa rasmi na Coastal Union ya jijini Tanga. 

Boban ambaye hivi karibuni alitangazwa kuachwa na klabu yake ya zamani Simba SC amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwachezea 'Wagosi wa Kaya'.

Boban aliwahi kuichezea Coastal Union mnamo mwaka 2000 ambapo alidumu hapo kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Moro Utd mwaka 2001.


(Chanzo: Shaffih Dauda Blog)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo