UBOVU WA MIUNDOMBINU WASABABISHA UKUSANYAJI MAPATO YA HALMASHAURI YA MAKETE KUSHUKA


Halmashauri ya wilaya ya Makete imeshindwa kufikia lengo lake la kufikia makisio ya mapato ya ndani ya shilingi 276, 340,000 katika kipindi cha Januari – Aprili 2013, na badala lake imefanikiwa kukusanya milioni 104 ndani ya kipindi hicho

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Makete ya Makete Mh. Josephine Matiro wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali katika wilaya yake kwa kipindi cha Januari-Aprili mwaka huu

Mkuu huyo ametaja sababu zilizopelekea halmashauri kutofikia lengo lake la kukusanya mapato hayo kuwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ikiwemo barabara nyingi kutopitika kutokana na mvua zilizonyesha wilayani mwake, hali ya hewa kutoruhusu pamoja na wafanyabiashara wengi kusitisha biashara zao ikiwemo mbao na viazi kutokana na maeneo mengi kutofikika

“baadhi ya wafanyabiashara walisitisha kufanya biashara zao kama mbao na viazi kutokana na maeneo wanayofanyabiashara kutofikika kiurahisi” alisema Matiro

Amesema kutokana na halmashauri kutofikia malengo hayo baadhi ya barabara zitakarabatiwa msimu huu ili zipitike na kufikia maeneo yote waliyoshindwa kuyafikia pamoja na kuongea na wakala wa barabara Tanroads mkoa wa Njombe kukarabati pia barabara zile zilizopo chini yao

Mkuu huyo wa wilaya amejiwekea utaratibu wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali kila baada ya miezi mitatu ambapo huitoa kwa wananchi wote wa wilaya yake ambapo katika taarifa hiyo hujumuisha sekta zote ikiwemo kilimo, afya, maji, elimu,barabara, maliasili na utalii


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo