MWENYEKITI WA NCCR-MAGEUZI NGARA AJIUZULU

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa James Mbatia
--
Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Kenned Staford Festo amejitoa katika uongozi wa chama hicho kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mwelekeo katika kuwahamasisha wanachama na wananchi kwa ujumla kuondoa changamoto zao katika kujipatia maendeleo wilayani humo.

Mwenyekiti huyo amechukua uamuzi huo jana baada ya kamati tendaji ya chama hicho mkoani Kagera kumsimamisha kwa muda wa miezi miwili iliyopita tangu Februari 20 mwaka huu ikidaiwa alishiriki maadhimisho ya miaka 36 ya CCM wilayani Ngara.
 
Akitangaza kujiuzulu Mei 2, Staford alisema amechoka kutumikia chama kisicho na ruzuku ya kuchangia maendeleo na ametumia gharama nyingi kuwahudumia wanachama huku akikosa nguvu kutoka kwa viongozi ngazi ya taifa akiwamo Katibu wa Chama hicho Taifa, Samweli Ruhuza. 
(Shaaban Ndyamukama)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo