JB - BONGE LA BWANA KITAANI


jACOB Stephen
JB mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jacob Stephen ‘ JB’ baada ya kutesa katika filamu ameibuka na utambulisho wa mradi mwingine wa mavazi JB ametengeneza fulana, top, kofia, mifuko ikiwa na nembo yake anayoipenda ya ‘Bonge la bwana’ nguo hizo zinapatikana katika maduka mbalimbali ya Jijini Dar es salaam na baadhi ya mikoa.
 

Jacob Stephen
JB msanii wa filamu Swahiliwood.
Jacob Stephen
JB akiwa na moja ya tuzo zake za uigizaji bora wa filamu.
 
Akiongea na FC meneja wa msanii huyo Marco Kilo amesema nembo ya msanii huyo mkubwa katika tasnia ya filamu ni yenye ubora wa hali ya juu na wameamua kutoa hiyo kwa ajilio ya wapenzi wa filamu ambao wanamhusudu sana JB ikiwa kama ni sehemu ya zawadi yao kwa wapenzi wa filamu na wadau wa filamu Bongo. 

“JB ni kipenzi cha watu, kuna wakati ambao wengi upenda kupiga naye picha wakionyesha mapenzi na msanii wao, kama uongozi tumepokea maoni mengi wakitaka JB aweze kutoa mavazi kwa ajili ya kuitangaza nembo yake ya Bonge la Bwana nasi kwa kuheshimu hilo tumefanya hivyo,”anasema Killo.

Wapenzi wa filamu wataweza kujipatia tishirt, Top na vitu vingine katika maduka mbalimbali ikiwa na alama ya JB bonge la bwana ikiwa katika ubora wa kipekee, tumuunge mkono msanii wetu katika kujiimarisha na kuongeza kipato.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo