Mifereji ikiwa imeziba na maji yanapita juu ya barabara
Kalavati hili limeziba na maji hayapiti, lakini hupita juu ya barabara na kuja kutumbukia hapa
Maji yanavyoharibu barabara kwa kupita juu badala ya kwenye kalavati
Uharibifu wa barabara zilizopo wilayani Makete umebainika ambapo mtandao huu umebaini kuwa chanzo kikuu cha uharibifu huo ni uzibaji wa mitaro ya maji iliyopo kando mwa barabara hiyo, jambo linalosababisha maji kupita juu ya barabara
Hali hiyo inasababishwa na wingi wa mvua zinazonyesha wilayani hapo, na mtandao huu unashauri wahusika kuona namna ya kuzibua mifereji hiyo ili maji yapite la sivyo maji yatazidi kupita juu ya barabara na kuziharibu