Na Ibrahim Yassin,Rungwe
KATIKA hali isiyokuwa
ya kawaida iliyowashangaza wengi imetokea baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika
kwa jina la Neema Abel Masebo (26) mkazi
wa kijiji cha Igogwe kata ya Bagamoyo
wilayani Rungwe mkoani Mbeya kubadirika ghafla kuwa mlemavu wa ngozi yaani (Albino),
Akisimulia mkasa huo Neema
masebo alisema kuwa alipatwa na kisa hicho siku za hivi karibuni wilayani Rungwe alipokuja kuwasalimia wazazi wake akitokea jijini Mbeya alikokuwa anaishi,na kwamba alipo lala
siku ya kwanza hasubuhi yake aliamka
akiwa amevimba mwili mzima,
Alisema kuwa mama
yake mzazi Tumaini Mlawa alipoona hali hiyo alimkimbiza katika hospital ya
wilaya ya Rungwe (Makandana)kwa ajili ya matibabu ambapo alilazwa siku 7 lakini
hali yake ikaanza kubadirika kuwa mbaya huku
ngozi yake ikianza kuchubuka taratibu hadi alipobadilika na kuwa mlemavu wa ngozi yaani (Albino)
Aliendelea kusema
kuwa baada ya madaktari kushindwa kuzuia hari hiyo
isiendelee alifika mganga wa hospitali ya serikali ya Marekani,Dr,Jescar akiwa katika ziara ya kikazi katika hospitali
hiyo alimchukua vipimo na kuvituma nchini kwake kwa uchunguzi zaidi lakini
hakuletewa majibu,na badala yake alipewa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua na
kuondoa vidonda,aina ya AQUASPORT
LOTION,ambayo yamemsaidia kutokuwa na
vidonda,
Alisema kuwa mara baada
ya kupewa mafuta hayo alitoka hospital
huku tayari akiwa na ulemavu huo,ndipo alipotokea mama mmoja jirani yake ambaye jina lake halikutajwa,alimpeleka
kwenye kanisa la maombi la Temple of prayer for all nations church,la wilayani
Kyela,na baada ya kufanyiwa maombezi ikiwa ni pamoja na kupakwa mafuta ya upako hali yake imeanza kurejea taratibu,
Baadhi ya wakazi wa kata ya bagamoyo wilayani Rungwe wamelihusisha tukio hilo na
imani za kishirikina huku wakisema toka dunia hii ilipoanza hawajawahi kuona
tukio kama hilo la mtu wa kawaida kubadilika ghafra kuwa na ulemavu wa ngozi
yaani Arbino,na kuwa wanamuomba mungu ili amsaidie na hali yake irejee kama zamani,
Mchungaji wa kanisa
hilo Nabii Charles Mkuvasa amekili kumpokea mgonjwa huyo kanisani kwake
na kwamba alipoletwa na mama huyo
alikuwa na hali mbaya lakini baada ya
kumfanyia maombi na yeye kupokea uponyaji
kutoka kwa yesu kristo,hali yake sasa imeanza kurejea taratibu na mungu yupo pamoja naye atarejea na kuwa
kama zamani.
