Imesemekana kuwa uvunaji
wa samaki umeongezeka kwenye Wilaya ya Babati Mkoani Manyara ambapo
mwaka 2005 walikuwa wanavua kiasi cha tani 102 na sasa wanavuna tani 208
za samaki.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Khalid Mandia wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM kwa mwaka 2005/2015 kwa waandishi wa habari na wakuu wa idara wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Alibainisha kuwa
pamoja na kufunga mabwawa hayo kwa miezi sita kisha wanayafungua pia
wameanzisha na kuimarisha vikundi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi
katika mialo.
Aidha kwa upande wa sekta ya nyuki idadi ya wafugaji nyuki alisema
kuwa imeongezeka kutoka wafugaji 1,474 mwaka 2002 hadi wafugaji 2,774
mwaka 2012 na nta kilo 2,532 zinazalishwa kwa mwaka.
Aliongeza
kuwa matumizi ya mizinga ya kisasa imeongezeka kutoka mizinga 199 mwaka
2005 hadi mizinga 5,780 mwaka 2012 wakati kiasi cha asali kimeongezeka
kutoka kilo 24,313 mwaka 2005 hadi kilo 67,832 kwa mwaka 2012.
Aliendelea kusema kuwa sekta
ya elimu imekuwa na mafanikio mwaka hadi mwaka kwani madarasa ya awali
shule ya msingi yameongezeka na shule za sekondari mwaka 2005 zilikuwa
30 na hadi mwaka 2012 zilifikia shule 41.
Alisema
kuwa kwa upande wa sekta ya maji asilimia 70 ya wakazi wa mji wa Babati
wanapata maji safi na salama na asilimia 60 ya wakazi walio nje ya mji
wanapata maji safi na salama.
Aliendela kusema kuwa mwaka
2005 walikuwa na hospitali mbili,vituo vya afya vinne na zahanati 17 na
mwaka 2012 walikuwa na hospitali tatu tatu,vituo vya afya tisa na
zahanati 39.
Alimalizia
kwa kusema kuwa ili kuendelea kusimamia sheria ndogo za uvuvi wenye
lengo la kuongezeka kwa samaki,wilaya hiyo inaendelea kuyafunga maziwa
na mabwawa waliyonayo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni kila
mwaka ndipo huyafungua.
