MAMA MZAZI WA SHARO MILIONEA AMKANA MSICHANA ANAYEDAI KUWA NA MIMBA YA SHARO



MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefungukia gari aliloacha mwanaye pamoja na mimba ambayo inadaiwa ni yake. 

Akizungumzia  suala la gari, Mama Sharo amesema: “Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.

“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala mpenzi.”

Sharo Milionea alifariki dunia Nov 26, mwaka jana kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Tanga.

Siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi wa Sharo na ana ujauzito wake


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo