Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akimsalimia
Mwezeshaji wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Asina Omari (kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia awamu ya
pili mjini Morogoro leo. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa
Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Pereira aliwataka maafisa wa jeshi
hilo wahakikishe msongamano ndani ya magereza nchini unapungua.
Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba
fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Pereira Ame Silima ili afungue mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na
maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza kabla ya kufungua mafunzo ya
jinsia kwa maafisa hao.
Maafisa
Magereza wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
nchi, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba
ya ufunguzi wa mafunzo ya jinsia mjini Morogoro.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa katikati
waliokaa) akiwa na Viongozi watendaji, maafisa wa Jeshi la Magereza,
wawezeshaji wa mafunzo ya Jinsia, na watumishi raia wa jeshi hilo katika
picha ya pamoja baada ya ufunguzi mafunzo hayo.
PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI