Wasamaria wema wakikifuta uchafu kichanga kilichokutwa kimetupwa maeneo
ya Kimara Baruti Bondeni karibu na maeneo ya Ubungo Kibangu.Yawezekana
mtoto huyo alitupwa asubuhi kwa sababu amekutwa akiwa hai na bado akiwa
na damu.Baada ya polisi kufika eneo la tukio Wasamaria wema
walimuwahisha mtoto huyo hospitali ya Palestina Sinza.
Kichanga hicho baada ya kufutwa futwa na kufunikwa.Mmoja wa wasamaria
wema ameniambia kuwa kichanga hicho cha kiume anaendelea vizuri baada ya
kupatiwa huduma katika hospitali ya Palestina na amepelekwa hospitali ya
Mwanyamala ambapo ndio kuna kitengo cha kuhifadhi watoto wachanga.
Inasikitisha sana jamani vyombo vya sheria vitoe adhabu kali kwa wanaofanya vitendo hivi ili kukomesha tabia hii.
CHANZO: ANAPETER.COM