
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye
makazi yake mkoani Dodoma jana kuhusu hatua zilizochukuliwa kudhibiti
vurugu za gesi mkoa wa Mtwara.Kulia ni waziri wa Mambo ya Ndani, Dk
Emmanuel Nchimbi.Picha na Fidelis Felix
---
MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi
kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa
kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa Rais
Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.
Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.
Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi mkoani humo.
“Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja,” alisema Pinda na kuongeza:Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea......>>>>