Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye
akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kasulu Mjini mkoani Kigoma.
Nape akizungumza kwa niaba ya CCM Wakuu wa wilaya chini watakaoshindwa
kusimamamia watendaji wa halmashauri wakiwamo wa vijiji ambao wanajiona
wao ni miungu watu mbele ya wananchi na kutamka bayana kuwa huu si muda
wa kubembelezana katika kuwatumikia wananchi.
CCM
imesema kuwa kutowajibika kikamilifu kwa watendaji na wakuu wengine wa
idara kwenye halmashauri nchini kumefanya wananchi kukichukia chama
hicho kwa kukosa huduma mbalimbali kutokana na uzembe wa watu wachache
na sasa wakati wao umefika.
Wananchi wa Heru Juu wakimsikiliza kwa makini Katibu wa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Nape akihutubia katika Mkutano wake katika Kijiji cha Karunga Kata ya Heru Juu, Wilayani Kasulu.
Nape
pia alipata fursa ya kuzungumza na wanachuo wa Chuo cha Ualimu Kasulu
na hapa Mmoja wa wanachuo hao Amina Mrisho akiuliza swali.
Nape
pia alipata fursa ya kuzungumza na wanachuo wa Chuo cha Ualimu Kasulu
na hapa Mmoja wa wanachuo hao Amina Mrisho akiuliza swali.
Wataalam
wa kwaito waliungana na Katibu wa Itikadi na Uenzei wa CCM, Nape Nnauye
kuburudika na picha ya chini ni wakali wanne ambao walipata zawadi ya
mshiko.
Wakazi wa Kasulu Mjini na vitongoji vyake waliofurika kumsikiliza Nape Nnauye.
Nape aliungana na wanamuziki wa Katag Sound bendi matata ya mjini Kasulu kucharaza nyuzi za gitaa kutoa burudani.
Miongoni mwa kazi alizofanya pia ni kukabidhi kadi kwa wanachanma wapya wa CCM mjini Kasulu.







