Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao.
FELA
Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ametoa
mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.
Mtu huyo
ambaye anatumia jina la mwanamuziki aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati
Fela Anikulapo Kuti, amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa
lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba wanaweza kuoa wanawake
wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa kwa waumini wa madhehebu
ya Kikristo barani Afrika.
Ndoa hiyo ilifungwa kama kawaida, ambapo
watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake, wakishuhudiwa na watu
kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo akinukuu vifungu vya Biblia
ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.
Tukio hili limeleta mkanganyiko
mkubwa na kuwaacha watu wengi wakijiuliza mengi kuhusu madhehebu ya
Kikristo yanavyojiingiza katika matendo yasiyoendana na imani yao,
ambayo inasisitiza mke au mume kuwa na mwenza mmoja
|