BUNGE LIINGILIE KATI KUWEZESHA UFUMBUZI WA MGOGORO WA GESI MTWARA.
SPIKA ATUMIE MAMLAKA YAKE KUELEKEZA KAMATI ITAYOKUTANISHA SERIKALI NA
WANANCHI. RAIS NA SERIKALI WAJISAHIHISHE NA KUONDOA UDHAIFU BADALA YA
KUENDELEA KULAUMU NA KUPOTOSHA
Nimemwandikia barua Spika atumie mamlaka na madaraka yake kutoa nafasi Bunge liingilie kati kuwezesha ufumbuzi wa mgogoro unaoendelea kati ya Serikali na wananchi kuhusu utafutaji, uvunaji, usafirishaji na utumiaji wa gesi asilia kutoka Mtwara.
Katika hatua ya sasa Serikali ni kupitia Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake ni sehemu ya watuhumiwa na washutumiwa hivyo ni muhimu majadiliano kati ya Serikali na wananchi kuwezesha ufumbuzi wa mgogoro huo yakasimamiwa na muhimili mwingine kwa dola.
Rais naye tayari ameshachukua upande bila kusikiliza kwa kina na kuyaelewa madai ya wananchi hivyo katika hali ya sasa ni muhimu kurejea katika madaraka na mamlaka ya wabunge kwa mujibu wa katiba ya nchi kuwezesha ufumbuzi wa mgogoro huu kuepusha hali tete inayoweza kuzuka na kuathiri uchumi na usalama katika maeneo husika.
Katiba ya Nchi Ibara ya 63 (2) inaelekeza kwamba sehemu ya pili ya Bunge (inayoundwa na wabunge) itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba.
Ili kuliwezesha Bunge kutumia mamlaka na madaraka hayo katika Mkutano wa Kumi wa Bunge unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu wa Januari 2013 katika kipindi hiki ambacho Nchi haina Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, nimemwandikia barua Spika atumie mamlaka na madaraka yake mujibu wa Kanuni ya 116 na Kanuni ya 114 fasili ya 14 ya Kanuni za Kudumu za Bunge kuelekeza mgogoro huu ushughulikiwe na Kamati mojawapo ya kudumu za Bunge wakati wa vikao vinavyoendelea hivi sasa Dar es salaam na vitavyofanyika Dodoma ili pande zote mbili; serikali na wananchi ziweze kuitwa kueleza madai na maelezo yake ufumbuzi wa haraka uweze kupatikana. KUSOMA ZAIDI BONYEZA HAPA>>>>>>>>>