HALI YA SINTOFAHAMU YAIKUMBA JIJI LA ARUSHA

Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
Hali ya sintofahamu imeibuka mkoani Arusha Baada ya Mbunge wa Arusha Mjini kuifunga shule ya sekondari Korona  hivi juzi ambapo hivi leo Mkuu wa Wilaya ya Arusha  Bwana John Mongela amefika shuleni hapo na kufanya kikao cha dharura na wazazi,walimu  pamoja na  baadhi ya watendaji wa halmashauri na kutangaza kuwa shule hiyo haijafungwa .

Aidha huyo Mkuu wa wilaya amekielezea kitendo hicho kuwa ni kutokuwa  na uelewa wa kutosha kuhusu sheria na kufafanua juu ya watu wenye mamlaka ya kufungia shule, ameeleza kuwa kitendo cha Mbunge huyo kuifunga shule hiyo ni kinyume cha sheria na utaratibu na mamauzi yeyote yanayotolewa kinyume na sheria ni batili akitolea mfano sheria namba 25 ya mwaka 1978  iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1995 inaeleza watu wenye mamlaka ya kufunga shule ni Mkaguzi wa shule,Mkuu wa Mkoa,Afisa elimu,Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi.
 
Pia aliendelea kusisitiza kuwa jambo hilo si zuri kwani huleta mkanganyiko mkubwa baina ya wananchi na viongozi na kusisitiza kuwa mbunge huyo alipaswa kufuata taratibu za kisheria za kufunga shule hiyo kabla ya kuchukua uamuzi huo.
 
Kutokuwa na viongozi wenye uwelewa wa kutosha kuhusu sheria ni tatizo kubwa linaloweza kuleta uvunjifu wa Amani katika jamii hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arusha  mjini John Mongela wakati akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya kufungwa kwa shule ya Korona na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema”
Kufuatia kufungwa huko ndiko kuliko  mlazimu mkuu huyo wa mkoa kuwatoa hofu wananchi kwa kutoa ufafanuzi kuhusu wa kiseria kuhusu mwenye madeti ya kufunga shule.

Pamoja na mambo mengine yaliyoliyobaini ni shule hiyo kutokuwa na mkuu wa shule kwa mwaka moja ,kukatiwa maji kwa deni la shilingi laki”3 na elfu  80 na kutokuwa na bodi ya shule,hali iliyomlazimu kumuagiza kaimu mkurugenzi wa jiji Bw Omary Mkombole na afisa elimu wa sekondari  Bi Vailet Mlowosa kuhakikisha matatizo hayo yanapatiwa ufumbuzi  ikiwa ni pamoja na wanafunzi kuendelea na masomo  mapema juma tatu .
 
Nao  baadhi ya  wazazi akiwemo mwenyekiti wa wazazi  Bwana Mikidadi Omari  na Bi.Zainab Mgandidi wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuomba serikali itatue matatizo yanayoikabili shule hiyo ili kuboresha elimu inayotolewa shuleni hapo.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ameeleza kuwa alitoa agizo la kufungwa kwa shule hiyo ingawa alijua ni kinyume cha utaratibu na alifanya  hivyo maksudi ili haki ipatikane na matatizo ya shule hiyo yapatiwe ufumbuzi  ambayo amedai ni mengi tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2011.
 
Godbless Lema amesema kuwa ana taarifa za kuaminika kutoka kamati ya fedha ya jiji kwamba kuna zaidi ya shilingi milioni 200 fedha za maendeleo ya jiji zilizofika kwa kuchelewa kwa mwaka wa fedha wa 2011 na 2012,fedha hizo bado hazijawekwa kwenye bajeti na tayari kuna mapendekezo ya viongozi wa Halmashauri kuwa fedha hizo zikarabati uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid Karume pamoja na uwanja wa basket ball wa SOWETO jambo ambalo amelipinga vikali na kuitaka halmashauri ielekeze fedha hizo kwenye ujenzi wa bweni wa shule hizo,kuweka huduma ya maji ya uhakika na ulinzi.
 
“Mimi nawashangaa wanalalamika kuwa nimefunga shule watoto hawaendi shule wakati wana wiki tatu tangu awafungue shule hawajafundishwa na wengine wako kidato cha tatu ile hali hawana matokeo ya mtihani wa kidato cha pili.Kwa kufunga shule hii nimewakumbusha kuwajibika kama unavyoona leo wote wamaeacha kukaa maofisini na kuenda kuangalia matatizo ya wananchi na shule hiyo kitu ambacho kinahitajika katika uwajibikaji na uongozi bora.
 
Aliendelea kusema kuwa nia ya kufunga shule hiyo si kutunishiana kifua na viongozi wa mkoa bali ni kuhimiza utatuzi wa matatizo ya wananchi,akitolea mfano ukosefu wa usafiri ambapo wanafunzi hao hulazimika kutembea umbali wa kilomita 6 na zaidi ,na pia watoto 98 waliohamishwa shuleni hapo kinyamela .
 
Awali Shule hiyo ilifungwa kwa juzi na Mbunge huyo akiambatana na baadhi ya watendaji wa Halmashauri  kwa madai ya kuwa na mapungufu mengi likiwemo la kutokuwa na vyoo vya kutosha ,walimu  na maji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo