KAMPUNI YA MULTCHOICE TANZANIA YAIOMBA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) KUWACHUKULIA HATUA WANAORUSHA MATANGAZO PASIPO KUWA NA HATI MILIKI

Meneja Mwendeshaji wa Kampuni  ya Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu masuala mbalimbali ya kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya hiyo Barbara Kambogi.
Na Dotto Mwaibale

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeombwa kuwachukulia hatua za kisheria Kampuni na watu wanaorusha matangazo bila ya kuwa na  hati miliki ya kurusha matangazo hayo.

Hayo yalisema Dar es Salaam  na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice Tanzania Barbara Kambogi wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.

Meneja huyo wa kampuni hiyo inayosambaza vifaa vya DSTv nchini ameiomba TCRA  kuwachukulia hatua za kisheria mara moja watu hao.

Alisema kuna baadhi ya kampuni yamekuwa wakijiunganishia matangazo kutoka kwenye kampuni zinazorusha kwa kutumia satalaiti bila ya kupewa hati miliki.

"Tunaiomba  TCRA ihakikishe kuwa wale wote wanaorusha matangazo
hayo wanakuwa na hati miliki ya kumruhusu kuchukua matangazo kwenye
kampuni zinazotumia satalaiti ili waweze kurusha kwenye vituo vyao" alisema Kambogi

Meneja Mwendeshaji wa Kampuni hiyo Ronald Shelukindo alisema
kwa wateja  wanaotumia vifaa vya DSTv hawatakumbwa na mfumo wa kuingia kwenye digitali kwa kuwa kampuni hiyo ilishaingia kwenye mfumo huo tangu awali.


Alisema  wateja wao wanatakiwa walipe kabla ya muda wa matangazo
hayo kuisha ambapo watakaokuwa wamelipia mapema watapewe asilimia 10 hivyo wata weza kuona vituo vingi vya kurushia matangazo hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo