BINTI ANAUZA BIKIRA YAKE ILI APATE FEDHA ZA KUMTIBU MAMA YAKE


NewsImages/6745110.jpg
Rebecca Bernardo anainadi bikira yake

Mwanamke mmoja wa nchini Brazil mwenye umri wa miaka 18 ameiweka bikira yake sokoni akiinadi ili apate pesa za matibabu ya mama yake ambaye ni mgonjwa.
Rebecca Bernardo mwenye umri wa miaka 18 atafanya mapenzi kwa mara ya kwanza na mwanaume atakayetoa dau kubwa kwenye mnada wa bikira yake.

Rebecca ambaye ni mwanafunzi wa sekondari amedai kuwa amechukua uamuzi wa kuinadi bikira yake baada kuvutiwa na jinsi mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Catarina Migliorini mwenye umri wa miaka 20 ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliweza kupata kiasi cha dola 780,000 kwa kuiuza bikira yake kwenye mnada.

Rebecca alidai kuwa Catarina alipata wadau mbalimbali kutoka kona zote za dunia ambao walitaka kuivunja bikira yake na yeye pia anatarajia wanaume wengi watajitokeza.

Rebecca ameongeza kuwa anatarajia kutumia pesa zitakazopatikana kwa kuiuza bikira yake kwaajili ya gharama za matibabu ya mama yake ambaye hajiwezi kitandani baada ya kupooza mwili wake.

Rebecca ambaye ni mkazi wa mji wa Sapeacu, Brazil alidai kuwa alijaribu kufanya kazi za kuuza vipodozi na pia kama weita lakini kazi zote hizo hazikumpatia kipato cha kumwezesha kumudu gharama za kumtunza mama yake.

Katika mchakato wake huu wa kuinadi bikira yake, Rebecca amedai kuwa jumla ya wanaume watatu washajitokeza na dau kubwa hadi sasa ni dola 35,000.

Wakati baadhi ya wanawake wakifanya kama mradi kuzinadi bikira zao na kufanikiwa kupata madau makubwa, mwanaume mmoja wa nchini Urusi, Alexander Stepanov mwenye umri wa miaka 23 alidai na yeye pia ni bikira na hajawahi kufanya mapenzi alifanikiwa kujinadi na kufanikiwa kupata mwanamke aliyenunua bikira yake kwa kufanya naye mapenzi kwa dola 3,000.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo