
Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki Mpendae,Zanzaibar akipakizwa
kwenye gari kupelekwa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar tayari kwa
kusafirishwa kwenda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Dar es salaam
kwa matibabu zaidi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Mjini
Zanzibar juzi jioni. Picha Martin Kabemba.
--
PADRI Ambrose Mkenda ambaye alipigwa risasi Jumanne iliyopita,
mjini Zanzibar na watu wasiojulikana amekana maelezo yaliyotolewa na
polisi yakimtaja kuwa ni Mhasibu wa Kanisa Katoliki, Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amelazwa, Padri huyo alisema
wadhifa wake ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchungaji anayeshughulikia
masuala yote ya Kanisa Katoliki visiwani humo.
Alisema hakuwa mhasibu wa kanisa hilo kama
inavyoelezwa na kwamba taarifa hizo siyo za kweli.Hata hivyo, Padri
Mkenda alisema alikuwa akimsaidia mhasibu kwa kipindi cha miezi mitatu.
Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea........>>>>>