Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ludihani wilayani Makete amewataka wananchi kupunguza ulevi wa pombe uliokithiri kijijini hapo.
Afisa mtendaji huyo Bw.Dakta Jaska Mahenge amesema kuwa baadhi ya watu kijijini hapo hawazingatii muda wa kazi na kuanza kunywa pombe muda wote kuanzia asubuhi.
Bw. Mahenge ameongeza kuwa walevi hao huchukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kupelekwa katika baraza la kata na kutozwa faini kulingana na makosa yake ambapo baadhi ya watu hurudia na kuendelea na ulevi.
Aidha amezitaja athari ambazo hutokea baada ya ulevi ni kupigana, kufanya ngono zembe inayosababisha maambukizi ya Ukimwi pamoja na kushuka na kudidimiza uchumi kijijini hapo.
Hata hivyo Bw.Mahenge ameomba serikali kusaidiana pamoja na mashirika binafsi kutoa elimu kuhusu ulevi na madhara ya pombe kwa ujumla.
Na Hadija Sanga