NAPE AZOMEWA LEO, KISA MASWALI HAYA


Baada ya kumaliza kuhutubia watu wasiozidi 70, Nape alisikika akisema tofauti yangu na Mzee Slaa ambaye hajawahi kuwa hata katibu kata na hawezi kuwaruhusu kuuliza maswali,kwa sababu hawezi kuyatatua,ni kwamba mimi ndio msemaji wa chama tawala na akija mwingne ni feki,mimi ni kama baba naomba niwape nafasi muulize maswali. Watu wakajitokeza.

Swali la kwanza: Mh Nape, CCM ndio chama tawala,na hakuna chama kingne tena chenye serikali, tunafahamu kwamba nchi yetu inaendeshwa na sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria,lakn cha kushangaza sisi wafanyakazi wa mgodini hapa Kakola -Bulyanhulu tumekuwa tukifukuzwa bila taratibu za kisheria kufuatwa,mfano mimi niliwahi kuuliza swali katika kikao chetu tulichofanya hapa mgodini na waziri wa madini alipokuja mgodini, swali lilihusu maslahi yetu na hivyo nilijua nitafukuzwa na mapema kabisa nilimwambia waziri kuwa baada ya swali hli najua sitakuwa na kazi,na yeye mbele ya wamiliki wa mgodi ule na wafanya kazi wenzangu alinìhakikishia kuwa sitafukuzwa,lakini leo ninapoongea hapa tayari nimekwisha fukuzwa,na nimemtumia ujumbe waziri huyo wa CCM lakn hadi leo hajanitetea,je mhe Nape huoni kuwa serikali ya CCM imewekwa mfukoni na kampuni hii ya Barrick?

MAJIBU YA NAPE: Nataka nikuoneshe kuwa nafahamu tatzo hilo, kuna watu sita mmefukuzwa na nimewagiza wabunge wenu akiwemo Maige ambaye yuko hapa wawape ushrikiano ktk kudai haki zenu. Watu wakaguna.!

SWALI LA PILI, Mh Nape kumekuwa na tabia ya watu wakawaida kufungwa kila wanapokamatwa wameiba, lakn jambo hli limekuwa halitokei kwa mawaziri wanapokamatwa kwa wizi,na matokeo yake wamekuwa wakijiuzulu na kuendelea kukaa majukwaani kama ambavyo leo uko na Maige hapo jukwaani, je huoni kuwa huu ni uonevu zidi ya wanyonge?

JIBU LA NAPE. Serikali ya kikwete tangu iingie madarakani imepangua baraza mara 3,hii ni kithibitisho kuwa hatuvumilii ufisadi, na ukweli ni kwamba kuna mawaziri wameshtakiwa, wananchi wakasikika wakisema tunataka wafungwe si kushtakiwa tu.

Halafu wakazomea, wakati m/kiti wa mkoa ccm shinyanga bwana Mgeja alipofunga mkutano ule watu wale wasiozidi 70 wakaanza kuimba peoples power.,peoples power,na kuonesha vidole viwili! Na Nape akapanda Gx lake akitanguliwa na Maige akifuatiwa na Mgeja wote wakiwa ktk magari tofauti wakati wa kuondoka.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo