Mbunge wa viti maalumu CHADEMA, Rahel Mashishanga amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na kushushiwa kipigo na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Kipigo hicho inadaiwa amekipata asubuhi ya leo wakati alipokuwa akitembelea vituo vya kupigia kura kata ya Mwawaza ili kujionea zoezi hilo linavyoendelea.
Gari lake limepondwa mawe huku vioo vya gari hilo vikiharibiwa.
Amepigwa jiwe na kutenguka bega lake la mkono wa kushoto, na meno mawili inadaiwa huenda yameng'oka baada ya kupigwa jiwe pia. Dah hii ndiyo Tz yetu.