SERIKALI imesema kuwa kamwe haiwezi kumtegemea mwekezaji kwa kila kitu huku baadhi ya Mambo yanaweza kufanywa na wanajamiii wenyewe katika sehemu huska.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoani Mara Augustine Mgendi anaripoti kuwa Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw John Henjewele katika hafla ya kukabidhi Madawati kwa baadhi ya shule zinazozunguka mgodi wa ABG North Mara, Vifaa vya Shule kwa baadhi ya wanafunzi na baiskel ya Magurudumu matatu kwa watu watatu wasiojiweza.
Amesema kuwa pamoja na Misaada inayotolewa na Mgodi huo kwa Jamii lakini pia serikali inashukuru Mahusiano Mazuri yaliyopo katika Mgodi huo wa ABG North Mara na Jamii.
Mkuu wa Wilaya huyo ameushukuru Mgodi huo kwa kugundua hali ya Walemavu,kutoa vifaa vya Elimu huku akisema hiyo ni hatua moja mbele katika kuisaidia Jamii
Awali akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya Meneja mkuu wa Mgodi wa North Mara Bw Gary Chapman,amesema Mgodi huo ni miongoni mwa Migodi Afrika ambayo imekuwa ikiwekeza katika Jamii hasa katika suala la Elimu,Afya,Maji na Maendeleo katika Jamii.
Amesema Pamoja na kutotimiza mahitaji kwa shule za Sekondary kwa asilimia mia lakini watajitahidi kushirikiana na Jamii jiyo katika kujiletea Maendeleo.
Aidha Uongozi wa Mgodi huo umetoa Madawati zaidi ya 1000 kwa shule za Nyangoto na Matare zilizopo katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara huku Miradi yote Mitatu ya Elimu, msaada ya Baiskel na Madawati hayo ikigharimu kiasi cha shilingi milioni 188
