ANAYETUHUMIWA KWA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO


Askari Namba G.2573 Pacificus Cleophase Simon(23), afisa wa polisi mkazi wa FFU Iringa, anashitakiwa kwa mauaji kufatia sheria namba 196 kifungu kidogo (i) sura ya 16,marejeo ya mwaka 2002. 
 
Manamo tarehe 2/9/2012 katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alimuua kwa kukusudia Ndg, Daudi Mwangosi . 
 
Akisomewa shitaka na mwendesha mashitaka mkuu wa serikali MICHAEL LUENA mkoa wa Iringa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wilaya ya Dyness Lyimo, mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote. 
 
Upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kesi imeahirishwa na itatajwa tena tarehe 26/9/2012.
Chanzo: mjegwa.blogspot.com
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo