SIHA
Mwenyekiti wa chama
cha wananchi
[CUF]Wilayani Siha Mkoani Kilimanjoro amewataka viongozi wote Wilayani
humo
pamoja na madiwani kuhamasisha Wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya
afya [CHF]
ili waweze kupatiwa matibabu kwa uraisi zaidi
IDD Hamisi alitoa
kauli hiyo wakati
akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake jana
Alisema Wananchi
sasa wanatakiwa
kupewa elimu madhubuti juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo kwa kuwa
unasaidia wanapopatwa na matatizo pale wanapoumwa wakati hawana fedha za
matibabu
Alisema madiwani na
viongozi
mbalimbali wanatakiwa kua mstari wa mbele kuhamasisha Wananchi kujiunga
na
mfuko huo kwa kuwa ndiyo wanaoishi nao muda wote na wanafahamu vyema
mazingira
yao
"Nawaomba ndugu
zangu madiwani na
viongozi wengine tuhamasishe wananchi wetu kujiunga na mfuko wa bima ya
afya
ili waweze kupatiwa matibabu kiraisi na mahali popote" alisema
Alisema endapo
madiwani katika
harakati zao za kimaendeleo kwa wananchi wataonyesha ushirikiano wa
kuhamasisha wananchi hao kujiunga na bima hiyo basi itawezesha kujipatia
matibabu yao bila shaka
