Kemmy, kwa sasa maisha yake ameyakabidhi kwa Bwana


MWIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu na maigizo Swahiliwood, Julieth Samson Kemmy, kwa sasa maisha yake ameyakabidhi kwa Bwana baada ya kuokoka.

Sasa kila anapokuwapo anatamani kuwahubiria Injili wasanii wenzake na jamii inayomzunguka.

Kwa sasa msanii huyo anaonyesha kwa vitendo katika kumtangaza Masia, lakini anaamini kuokoka hakupingani na kazi yake ya uigizaji.

Hii ni kazi ambayo kama inatumika vizuri inaweza kusaidia jamii katika kubadilika na kutenda mema, si kila filamu lazima iwe na upotoshaji, alisema Kemmy.

Lakini pia ninaangalia uhusika wangu katika filamu, siwezi kuigiza filamu ambayo inapingana na neno la Mungu au hata kuigiza nikiwa na nguo ambazo hazikubaliki kijamii.

Kemmy ni moja kati ya wasanii waliolijenga kundi la Kaole Sanaa kwa uigizaji na utunzi wa maigizo yaliyoteka watazamaji wa televisheni.

Hivi karibuni ametunga filamu inayoitwa Diana ambayo anaamini kuwa ni filamu yenye ujumbe katika jamii.
SOURCE-MWANASPOTI


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo