Msanii maarufu wa bongofleva hapa nchini Diamond Platnumz amesema hajutii kuachana na mlimbwende Wema Sepetu
Diamond ameyasema hao wakati akihojiwa katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV&radio na kusema kwa hata Wema Sepetu mwenyewe naye hajutii kuachana na Diamond
"Unajua mpaka dakika hii ninavyozungumza na wewe sidhani kama kuna siku nitarudiana na Wema maana kwa sasa kila mtu anaendelea na ustaarabu wake" alisema Diamond
Pia Diamond amekanusha vikali kuwa anasafiria nyota ya Wema a.k.a umaarufu na mafanikio yake umesababishwa na Wema, na badala yake yeye amesema ndiyo aliye "mbusti" wema na kumfikisha hapo alipo kwani Wema alimkuta Diamond akiwa Super star tayari