Makete 08.02.2011
Wadau mbalimbali wa utekelezaji wa mradi wa Tmf ambao ni Wafanyakazi wa Kitulo Fm, PIUMA na MASUPHA wamejengewa uwezo wa namna ya kuandaa vipindi vya redio na namna ya kutekeleza mradi huo
Lengo la mradi huo ni kuongeza uelewa kwa jamii ya Makete juu ya Uchangiaji wa mila na desturi katika maambukizi ya VVU, matunzo na huduma kwa watoto yatima na wenye VVU kupitia vipindi vya redio
Akizungumza na washiriki hao mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Charles Kayoka amesema kuwa malengo ya mradi huo ni vyema yakatekelezwa kwa ufanisi unaotakiwa ili kuisaidia jamii ya wanamakete na wote watakaokuwa wakisikiliza vipindi hivyo
Aidha amewataka watangazaji hao kuandaa vipindi vilivyobora na vyenye kuigusa jamii kwa kuwashirikisha wanajamii wenyewe na wadau mbailmbali watakaohitajika
Kwa upande wao washiriki hao wamesema wako tayari kuutekeleza mradi huo ipasavyo na kuomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwao pindi watakapoanza kupita maeneo mbalimbali ya wilaya ya Makete ili kutekeleza mradi huo ikiwemo kuandaa vipindi