MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA UPIMAJI WA AFYA ULIOANDALIWA NA NHIF MKOANI RUKWA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipimwa urefu na mtaalamu wa mfuko wa bima ya afya ya jamii leo katika viwanja vya shule ya Sekondari msakila katika Manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni uzinduzi rasmi wa huduma hiyo ambayo inatolewa bure na mfuko huo katika kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko pamoja na kujali afya zao. 

Shirika hilo lipo katika maadhimisho ya miaka 10 ya utoaji huduma nchini. Katika hotuba yake fupi Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi waweze kujua afya zao na kupata ushauri ambao unatolewa bure.

Aidha aliwataka viongozi wa mfuko kutoa elimu ya afya kwa wananchi katika maeneo yote nchini haswa katika maeneo ya pembezoni kusaidia kupunguza gharama za mfuko zinazosababishwa na maradhi yanayoweza kuepukika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akipima mapigo ya moyo (BP). Vipimo vingine vinavyotolewa ni uwiano wa sukari mwilini na ushauri bure kwa wananchi watakajitokeza kupimwa.
Wananchi wengi wamehamasiku kupima afya zao kama inavyoonekana pichani, rukwareview.blogspot.com (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Na fullshangwe blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo