DKT. BILAL AZINDUA JUKWAA LA UCHUMI WA KIJANI LA SIKU 3 MKOANI IRINGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu Mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2012, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, Leo Mei 8, 2012, litakalofanyika kwa Siku tatu mkoani Iringa.
Msanii wa Muziki wa Asili na Mashahiri, Mrisho Mpoto, akighani maneno yake yenye ujumbe Kuhusu Utunzaji wa Mazingira, mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliofanyika Mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, mkoani Iringa leo.
Na moblog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo