JOHANNESBURG:
Vifaru 201 wameuawa mwaka huu nchini Afrika Kusini, na wawindaji haramu 165 wamekamatwa nchini humo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa takwimu za idara ya kulinda mazingira.
Afrika Kusini ndio nchi yenye idadi kubwa ya vifaru ulimwenguni. Wawindaji haramu 67 walikamatwa katika mbuga ya taifa ya Kruger, ambayo ni miongoni mwa mbuga kubwa zaidi za wanyama barani Afrika.
Uwindaji haramu wa vifaru umeongezeka katika siku za hivi karibuni, kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya pembe zao katika nchi za Asia.
Mwaka jana waliuawa vifaru 440, hiyo ikiwa idadi kubwa zaidi ya wanyama hao kuuawa katika kipindi cha mwaka mmoja.
DW