Wananchi wilayani Makete wametakiwa kutoa ushirikiano dhidi ya changamoto zinazowakabili waalimu pindi wanapotakiwa kufanya hivyo kwani kwa kufanya hivyo kutaleta ufanisi katika jamii
Hayo yamezungumzwa na baadhi ya maafisa ustawi wa jamii wilaya ya Makete walipofanya ziara katika shule ya msingi Makete na kubaini changamoto mbalimbali zilizopo shuleni hapo ikiwa ni pamoja na kukosekana ushirikiano baina ya wazazi na waalimu, uchache wa waalimu, pamoja na uhaba wa vitendea kazi ikiwemo vitabu na chaki
Changamoto nyingine zilizobainika ni pamoja na baadhi ya wawazi na walezi kukataa kuitikia wito pindi wanapoitwa shuleni kwa ajili ya vikao ama mazungumzo yanayohusu maendeleo ya watoto wao
Miongoni mwa Maafisa Ustawi hao aliyejitambulisha kwa jina la Denis Sinene amewaasa wanafunzi hao kuacha vitendo viovu ikiwa ni pamoja na kuacha utoro, na kuwataka kusoma kwa bidii
Na Aldo Sanga & Riziki Manfred