
WANAFUNZI WA VYUO VIKUU mkoa wa Dar es Salaam wameandamana hadi katika Ofisi Ndogo za CCM kupongeza hatua iliyochukuliwa na Kamati yaCCM huku wakiunga mkono na kutaka mawaziri waliotajwa kwenye kashfa waondolewe madarakani | ||
Jana wanavyuo hao walivamia ofisi hizo Mtaa wa Lumumba wakwia na mabango na baadhi yao yalisomeka ‘JK vunja ukimya, chukua hatua jenga chama na Taifa kwa ujumla,’ ‘Wasaidizi wa JK wajibikeni kabla ya kuwajibishwa,’ ‘ Wezi wasisimamishwe wafukuzwe na kuchukuliwa hatua. Mengine yalisomeka ‘Takukuru kuweni kama CAG’ na mengine mengi Wanavyuo hao walipokelewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye. Wanavyuo hao waliandaa risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Assenga Abubakari. Wanafunzi hao katika risala yao hiyo walitoa muda wa mwezi mmoja kwa Serikali iwe imewachukulia hatua mawaziri wote waliohusika vinginevyo shirikisho hilo litawatoa maofisini mawaziri hao. Akiwajibu wanafunzi hao Nape alisema tayari Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, imemshauri Rais Kikwete kuwa wahusika wote washughulikiwe na kufikishwa mahakamani ikiwemo na kusuka upya baraza lake la mawaziri. Alisema Ijumaa iliyopita, Kamati hiyo ilikutana jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete na kukubaliana kuwepo kwa mabadiliko katika Baraza la Mawaziri |