Askari wa wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa wamefanikiwa kukamata majangili 3,030 wakiwa na silaha aina ya Shotgun 15 gobore 239 na risasi 778.
Mkuu wa idara ya ulinzi katika hifadhi ya Ruaha Paul Gwaha aliyasema hayo wakati wa ziara ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari mkoani Iringa walitembelea hifadhi hiyo kama njia ya kuutangaza utalii wa mikoa ya kusini mwa Tanzania.
Alisema kuwa silaha hizo zimekamatwa katika misako mbali mbali inayoendelea katika hifadhi hiyo kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi sasa na kuwa jumla ya mikuki 77 ,kokoro 4337 na mitumbwi 1589 imekamatwa pia katika eneo hilo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Mkuu huyo wa alisema kuwa katika msako huo jumla ya nyavu 29,978 ,ndoano 70184 na siala nyingine mbali mbali zilizokamatwa katika misako hiyo ni 117,961.
Mkuu wa hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa Stepheno Qolli Alisema kuwa shughuli za ulinzi katika hifadhi hiyo zimekuwa zikifanywa na askari wa hifadhi kwa ushirikiano wa mradi wa ujirani mwema wa uhifadhi wa mali hai Idodi na Pawaga (MBOMIPA) .
Hata hivyo alisema kasi ya watalii wanaofika kutembelea hifadhi hiyo ya Ruaha bado si kubwa ukilinganisha na idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za kaskazini na kuwa bado kuna haja ya kuongeza nguvu zaidi katika kuzitangaza hifadhi hizo za mikoa ya kusini ikiwemo hifadhi ya Ruaha .
Kwani liasema kuwa hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ndio hifadhi inayoongoza kwa kuwa na wanyama wengi zaidi na ndio hifadhi ya kwanza kwa ukubwa Tanzania ila bado idadi ya watalii wanaofika kutembelea si nzuri sana.

Habari kwa hisani ya www.francisgodwin.blogspot.com