Baba amchoma mikono mwanaye, kisa kamkuta na elfu 5

Mtoto Elizabeth Mathias Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ziwani Mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita Mkoani Geita ameunguzwa mikono miwili kwa kulowekwa kwenye maji ya moto na Baba yake mzazi (jina halijatajwa) baada ya kumkuta akiwa na shilingi 5000 ambazo alishindwa kueleza alikozitoa.


Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amekiri kumkamata Mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo huku akisema Mtoto huyo amekuwa akilelewa na Mama yake wa kambo ambaye pia alishiriki katika kutekeleza tukio hilo.

Kamanda Safia amesema Jeshi la Polisi linaendelea kutoa rai kwa Wananchi kuacha tibia za kuwaadhibu Watoto kikatili na kusema atakayekaidi atachukuliwa sheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo