“Suala la Katiba limezungumzwa na kila Mtu kwa style mbalimbali kwa majina mbalimbali, kwa bahati nzuri mwaka jana nilikaa na Chama changu tukakubaliana nasi kuungana na Vyama vingine kutoa tamko la kukubali mchakato wa marekebisho ya Katiba”
“Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya Katiba kwa jinsi tutakavyokuja kukubaliana hapo mbele lakini tupo tayari kuukwamua, wengine wanasema tuanze na Katiba ya Warioba wengine tuanze na Katiba pendekezwa lakini ile ilikuwa mwaka 2014 ni miaka minane sasa kuna mambo kadhaa yameshabadilika”
“Kwahiyo kuna haja ya kuiangalia hali halisi ya sasa hivi, yale yaliyomo mule yanatufaa au hayatufai kwahiyo inawezekana zile mbili zote zikawa sio vyanzo vizuri vya kuanzia tukaanza tuliyonayo yapi mazuri yapi yarekebishwe lakini tukakopakopa kutoka kule na mengine ambayo hizo Kamati zitakazoundwa zitakuja nayo”
“Nataka niwape faraja kwamba hivi karibuni itaundwa Kamati ya kutushauri tuendeje ambayo itakuwa na Watanzana wa Sekta na Vyama vyote, Katiba hii sio ya Vyama vya Upinzani pekee, itakuwa Kamati ya Watanzania wote ili waje na kitu ambacho kitakuwa cha Watanzania, Katiba ya Watanzania” - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 03 januari, 2023
"Twendeni tukafanye Siasa za Kistaarabu, rekebisheni Serikali, isemeni Serikali onesheni mapungufu ili Serikali ijirekebishe na ifanye kazi yake,
Najua mtaenda kusema Serikali hii in madeni ni kweli lakini nenda kwenye uchambuzi Hayo madeni yamefanya nini usiseme tu ina madeni lakini sema Serikali ina madeni lakini Tunashukuru kwama sasa Reli wakandarasi mpaka Kigoma wapo,
Uongo haujengi lakini kweli inajenga kwahiyo niombe sana twendeni tukafanye mambo yetu kwa ustaarabu" - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 03 januari, 2023
"kama wastaarabu, watanzania wenye sifa ndani ya dunia hii Niwaombe sana ndugu zangu tunatoa ruhusa ya kufanya mikutano ya vyama vya siasa twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, tukafanyeni siasa za kupevuka tukafanye siasa za kujenga na si kubomoa" - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 03 januari, 2023
"Ni haki kwa vyama vya siasa kuendesha Mikutano yao ya Hadhara lakini ndugu zangu tuna wajibu, kwa upande wa serikali tumeshajipanga, wajibu wetu ni kulinda Mikutano ya vyama vya siasa mnatupa taarifa kama sheria na kanuni zinavyosema vyombo vinatoa ruhusa wakiona kuna hatari hawatoi ruhusa lakini kwa hatua tuliyofika ruhusa za kufanya Mikutano zitatolewa,"
"Wajibu wetu ni kuwalinda mfanye Mikutano yenu kwa usalama mmalize vizuri muondoke vizuri, wajibu wenu vyama vya siasa ni kufuata sheria na kanuni zinavyosema" - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 03 januari, 2023
"Mikutano ya Hadhara hii ni haki kwa sheria zetu, ni haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano yao ya hadhara, uwepo wangu leo mbele yenu ni kuja kutoa ruhusa, kuja kutangaza kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa." - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 03 januari, 2023