Alvera Uwitonze mkazi wa nchini Uganda (56) amesema anatafuta mume kwa sababu yuko mpweke na amechoka kufanya kila kitu pekee yake.
Alvera, ambaye anaishi na ulemavu uliomfanya ashindwe kutembea kawaida, amesema alikuwa na wachumba hapo awali lakini aliogopa kuchumbiwa, kwa kuhofia mwanaume angempa ujauzito na kumkimbia.
Alvera amesema kuwa anajuta kutowapa wanaume nafasi ya kuwa naye walipomkaribia akiwa msichana mdogo. "Walikuwa wakija hapa na kuniuliza wanioe nikawakatalia wote, niliogopa atakuja mwanaume kunipa ujauzito wakaniacha mimi na mtoto na kuendea mtu mwingine,".
Alifichua kwamba alipata mwanamume ambaye alikubali kumuoa lakini kwa masharti kwamba amlipe KSh 22,000. "Ninaishi ndani kabisa kijijini na hakuna njia ya kupata pesa za aina hiyo, lakini nikipata, bado nitampa kwa sababu niko mpweke na pia nataka kuwa na familia yangu,"
Alvera, aliyezaliwa bila hali yake ya sasa, alisema wazazi wake walimpeleka kwa mganga badala ya hospitali alipougua na kwa sasa anaishi pekee yake, akilima shamba lake, anajipikia na ana redio ya zamani ambayo inamsaidia kutoa upweke.
Alvera ameongeza kuwa wanaume wengi wanasema kuwa muda wa kumuoa umepita na wanapendelea wanawake wachanga na ambao hawana ulemavu.