Mchungaji ambaka shangazi wa mchumba wake

Jeshi la Polisi nchini Zambia, linamsaka Mchungaji wa Kikongo anayejulikana kwa jina la Mike Mapalo anayedaiwa kumnajisi mtoto wa miaka 13 na kisha kutorokea eneo ambalo basi sass bado halijulikana.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Copperbelt, Peacewell Mweemba amesema tukio hilo lilitokea Desemba 17, 2022 katika kitongoji cha Ndola kilichopo mjini Lubuto, majira ya saa 22:00 usiku.


Amesema, mtoto huyo mwathiriwa anatoka eneo la Luapula kuja Ndola kwa ajili ya likizo kumtembelea shangazi yake na likumbwa na makes huo baada ya kunajisiwa hali iliyopelekea kupata maumivu sehemu za siri.


Kamanda Mweemba amefafanua kuwa, “Siku hiyo ya maafa, shangazi yake hakuwepo nyumbani na msichana alikuwa amebaki na mshukiwa ambaye ni mpenzi wa shangazi yake na alitumia nafasi hiyo kukamilisha unyama alioutenda.” 


Aidha, inaarifiwa kuwa baada ya kitendo hicho, mtuhumiwa alikimbia na mwathiriwa alikwenda kumjulisha shangazi yake mwingine ambaye alitoa taarifa Polisi huko Lubuto huku taarifa zikionesha kuwa mshukiwa huyo amekimbilia nchini kwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo