Nabii awataka waumini wake kumchangia fedha anunue gari jipya

Nabii Samuel Kakande wa Kanisa la Synagogue Ministries nchini Uganda anatazamia kuanza mwaka mpya na gari jipya ambalo anasema waumini ndiyo watanunua.


Wakati wa ibada yake iliyopeperushwa mubashara hivi punde, mtumishi huyo wa Mungu alisema kuwa gari analoendesha kwa sasa lilinunuliwa na waumini lakini limezeeka na linahitaji kubadilishwa.


Alisema kwamba wale tu wanaompenda ndiyo wanapaswa kujitokeza kuungana ili apate gari nzuri, na kwamba Yesu atawabariki. "Nataka dola 300 pekee kutoka kwa kila moja. Tutachangisha, na kisha kununua gari nzuri. Ninaendesha gari huku nikiwaombea. Kuna ubaya gani hapo?" alihubiri.


Aliendelea na kunukuu kitabu cha Luka sura ya 6 ambayo inasema "Muwe wepesi wa kutoa nanyi mtapokea. Kipimo mtakachotoa mtar udishiwa kikiwa kimejaa na kushindiliwa na kutikiswa na kufurika. Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.” Kakande pia alifafanua kuwa waimuni pia wanaweza kuongezea katika hicho cha dola 300 (KSh 36,000) akisema wale walio tayari wanaweza kutoa kiasi kikubwa zaidi kulingana na uwezo wao.


Wafuasi wa nabii huyo walisema kuwa wako tayari kupata baraka na hivyo watashiriki katika mradi huo huku baadhi yao wakisema kuwa wangetamani kuchangia lakini hawana fedha.


Kakande anamiliki magari kadhaa ya kifahari kati yao ikiwemo Lexus LX 570 lililogeuzwa kukufaa mwaka 2017 na Mercedes Benz G-Class. Ombi la Kakande linakujia siku chache baada ya kumzawadi msanii chipukizi wa Kenya Sheila Sheldone na mama yake Vivian Otieno KSh 650,000 ili kukuza talanta yake.


Sheila na Vivian walikuwa wametafuta ukombozi kutoka kwa nabii huyo kwa kile wanachoamini kuwa ni nguvu za giza zinazowazuia wasifanikiwe.

Chanzo: TUKO.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo