Mbowe: Siwezi kupangiwa

Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amesema ameshangazwa kupigwa marufuku kutoa salamu ya vyama vingine katika mikutano ya uchaguzi inayoendelea kufanyika huku akidai sheria hiyo haipo bali ni sheria ya hofu

Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa yupo katika muendelezo wa kumuombea ridhaa mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia (CHADEMA), Salum Mwalimu kuwa Mbunge wa eneo hilo katika siku zijazo za usoni ambapo kwa sasa zimebakia takribani siku 12 tu uchaguzi mdogo kufanyika.
"Juzi kimeitishwa kikao ambacho kina mashitaka dhidi ya CHADEMA na mengine ni wanaopenda haki katika taifa hili. Kikao kile kikaamua kwamba kwenye mikutano iwe ni marufuku kusalimiana kwa salamu za chama kingine", amesema Mbowe.
Pamoja na hayo, Mbowe ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema "nikashangaa kidogo, tukija kwenye mkutano hapa Kinondoni hatuji kuzungumza na wanachadema peke yao maana uwanja huu  wapo wanawacuf, wanaccm sasa iweje uniambie Mbowe usitoe salamu ya CUF katika mkutano. Hiyo sheria katika uchaguzi haipo ni sheria ya hofu kwa hiyo mimi natambua uwanjani hapa wapo wanacuf na nina haki ya kuwasalimia wote".
Kwa upande mwingine, Mbowe amesema kusalimia ni hiari yake hivyo hawezi kupangiwa kufanya hivyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo