Taarifa kutoka Momba mkoani Songwe zinaeleza kwamba askari polisi wa kitengo cha usalama barabarani mwanaume ambaye jina lake halijawekwa wazi mwenye umri wa miaka 29 anadaiwa kumuua mpenzi wake kwa kumchinja na kitu chenye ncha kali.
Tukio hilo kusikitisha limetokea juzi Jumamosi Januari 6,2018 asubuhi jirani kabisa na kituo cha polisi Kamsamba kilichopo tarafa ya Kamsamba wilaya ya Momba mkoani Songwe ambapo askari huyo alikwenda kutekeleza unyama huo kwa mpenzi wake Winfrida Bedwin Lucas ambaye ni muuguzi katika kituo cha afya cha Kamsamba .
Baada ya ofisa huyo wa polisi kutimiza haja yake inasemekana kwamba alikuwa kazini katika kituo hicho cha Kamsamba na alikwenda katika ghala la silaha na kuchukua bunduki kisha kujipiga risasi ya shingo na maisha yake yakaishia hapo hapo.
Mtoa taarifa wetu anaeleza kwamba chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi ambapo askari polisi alikuwa akimtuhumu mpenzi wake huyo (nesi) kutokuwa mwaminifu na kuwa na mahusiano na wanaume wengine.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa askari huyo alikuwa anamtaka kwa nguvu kumuoa mwanamke huyo.
"Winfrida alikuwa nesi katika kituo cha Afya kamsamba,ameuwawa kwa kuchinjwa kama kuku na askari polisi-kituo cha polisi Kamsamba, alikuwa anamtaka kwa nguvu kumuoa na kukataliwa,akaenda akaanua nguo za binti na akampigia simu aende akachukue nguo zake alipofika pale jamaa akamkamata akampiga kisu na yeye kwenda ofisini akachukua bunduki akajiua",kimeeleza chanzo chetu kingine cha habari.