Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Mrema amesema yeye ni mzima wa afya na hata ugonjwa amabo ulikuwa ukimsumbua kwa miaka mingi ameshapona.
“Afya yangu ni njema ni kweli nilikuwa mgonjwa tangu mwaka 2015, wakati wa kampeni na wakawa wanasema msimchague Mrema ni mgonjwa ni marehemu Mtarajiwa, ila tangu Magufuli kushika urais wake aliahidi serikali itasimamia matibabu yangu, nikapelekwa India na ile kansa iliyokuwa inanisumbua imepona kabisa”, amesema Lyatonga Mrema.
Mrema ameendelea kwa kusema kwamba...”kwa kweli naona mambo yangu ni mazuri hata sura inang'aa, ngozi ile iliyokunjamana haipo tena. Leo asubuhi nimepata taarifa kuwa kuna kikundi kile kile cha 2015 wanataka nife, wanahisi naelekea tena Vunjo kuchukua lile jimbo, lakini nataka kuwaambia mimi sio mgonjwa kansa nimepona, hajafa mtu hapa”, amesema Lyatonga Mrema.
Leo asubuhi kulikuwa na taarifa kuwa mwanasiasa hyo amefariki dunia, kitendo ambachosio mara ya kwanza kutokea kwa kiongozi huyo, ambaye sasa anashikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini.