Mkandarasi VETA Makete amchefua Waziri Prof. Ndalichako

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof Joyce Ndalichako ameonesha kutoridhishwa kwake na ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu katika chuo cha ufundi VETA Makete baada ya kufanya ziara chuoni hapo hii leo
Waziri Ndalichako amesema mkandarasi anayejenga majengo hayo ambaye ni wakala wa Majengo nchini (TBA) analeta masihara na kazi ya serikali ya awamu ya 5, ambapo tangu akabidhiwe kazi hiyo Oktoba Mwaka jana hii leo ndio ameanza kazi ya kusafisha uwanja kwa ajili ya ujenzi huo
Akipatiwa maelezo ya mradi huo ambayo hayakumridhisha kutoka kwa Mkandarasi huyo, waziri Ndalichako amesema kwa sasa hana imani na TBA kutokana na kuonesha kukwamisha kazi alizopewa na serikali katika maeneo tofauti hapa nchini
Waziri Ndalichako ametilia shaka gharama zitakazotumika kujenga nyumba za walimu ambapo nyumba moja inatarajiwa kujengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 160 jambo ambalo amesema ni gharama kubwa kuliko serikali inavyotaka
“Sisi wizara ya elimu tumekuwa tukijenga nyumba za walimu kwenye shule mbalimbali hapa nchini kwa kati ya shilingi milioni 60 hadi 70, sasa iweje hapa iwe milioni 165, mbona mnajenga nyumba za kifisadi?” amesema Ndalichako
Pia ameshangazwa na taarifa inayoainisha kuwa gharama ya ujenzi wa bweni moja la kubeba wanafunzi 40 utagharimu zaidi ya shilingi milioni 300 na kusema hayuko tayari kutoa fedha hizo kwa kuwa ni kubwa kupita kiasi
Amesema wizara yake ina fedha nyingi kwa ajili ya kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa hivyo hakuna kisingizio cha kukosa fedha
“Meneja wa kanda, kama mtajenga bweni kwa fedha hii nakuhakikishia huna kazi, hii fedha ni nyingi mno” amesema Waziri
Hata hivyo mkandarasi huyo amemuomba na kumhakikishia waziri kuwa atajitahidi ujenzi huo ukamilike kabla ya muda uliopangwa, hivyo waziri amuamini kwa hilo, jambo ambalo Mh Ndalichako amelitilia shaka na kusema hana imani na TBA na wakitaka imani yake irejee waifanye hiyo kazi kwa vitendo
Katika hatua nyingine waziri huyo amekagua majengo ya chuo hicho na kuridhishwa na ujenzi wake wa kiwango, ambapo amesema licha ya mkandarasi aliyejenga majengo hayo kusimamishwa kwa kukiuka sheria ya manunuzi, lakini alijenga vizuri na kusema anastahili kurudishwa na aendelee na kazi, kwa kuwa anatambua thamani ya fedha ya serikali

“Ni afadhali huyu aliyejenga haya majengo ya VETA karibia 8 na ameyajenga kwa kiwango halafu amesimamishwa kwa kukiuka taratibu za manunuzi, lakini ni bora huyu anayekiuka taratibu za manunuzi lakini kajenga majengo mazuri kuliko hawa wanaotaka kujenga kwa gharama kubwa halafu wanasuasua, mimi naagiza arudishwe
 Mkandarasi huyo akieleza jambo kwenye ziara hiyo ya Waziri Prof Joyce Ndalichako
 Waziri wa elimu Prof Ndalichako (kulia) akikagua eneo linapojengwa nyumba za walimu wa chuo cha VETA Makete
 Mtambo ukiendelea kusafisha eneo la ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi Chuo cha VETA Makete
 Waziri Ndalichako akimtahadharisha Mkandarasi wa ujenzi huo
Ukaguzi wa waziri Ndalichako ukiendelea


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo