Wakurugenzi kukatwa mishahara

Katibu mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Lauren Ndumbaro amewataka wakurugenzi, wakuu wa idara na watumishi wote kuwa wazalendo na kuwatumikia vyema wananchi

Katibu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa manispaa ya Songea, ambapo ameeleza kuwa, ni lazima kila mtumishi atimize majukumu yake ili kurahisisha majukumu ya mwingine kwani idara nyingi zinategemeana kiutendaji.
“Kila mtumishi inabidi ajitathimini abadilike awe mwadilifu zaidi, awe mchapakazi zaidi, awe binadamu zaidi na awe mwaminifu zaidi”, amesema Ndumbaro.
Aidha Dkt. Dumbaro amewataka Wakurugenzi na Maafisa utumishi kushughulikia na kuyatatua matatizo ya watumishi na endapo hawatafanya hivyo basi wizara itasimamisha mishahara yao ili nao wapate usumbufu kama wanaopata watumishi wa kawaida.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo